Viongozi mbalimbali nchini wameibua hisia kali kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja almaarufu LGBTQ.Baadhi ya mapendekezo ambayo yametolewa na viongozi hawa ni kuwa,yeyote aatakayehusishwa na visa hivi anatarajiwa kufungwa zaidi ya miaka kumi na adahabu nyingine.
Ikiwa mshtakiwa atapatikana na na hatia,basi atafungwa miaka ishirini.Zaidi ya z itakuwa ghali mno kama ikiwa mkosewa atakuwa mtoto ama mtu aliye na upungufu wowote, kwani,mshtakiwa atahukumia adhabu ya kifo.
Kukwamua uwezo wa nchi wa kushughulikia maswala ya ndani na nje ya nchi ni mojawapo ya matakwa ya shinikizo jinsia anavyosema Mbunge wa Homabay mjini,Peter Kaluma.
Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya ndizo asili ya jamii hii,na kuikubali kama mojawapo ya haki za haki za binadamu.Hata hivyo,nchi za kiafrika kupitia viongozi wake, zimepinga vikali pendekezo hili na kuiona tabia hiyo kama inayoenda kinyume na mienendo ya jamii za kiafrika.