Familia hiyo kutoka eneo bunge la Kabuchai maeneo ya Mukhoya  imeshuhudia upasuaji wa mwili wa mpendwa wao aliyepoteza maisha yake kwenye hali tatanishi.Andrieta Nakhumicha mwenye umri wa makamu alifariki tarehe nane mwezi huu mwendo wa saa nne akiwa afisini mwa chifu wa eneo hilo la Kabuchai.

ups

Familia inaashiria marehemu alifariki baada ya kuanguka kwenye afisi hiyo walimokuwa wakiendeleza kesi ilyokuwa ikimkabili.Na walipomkimbiza zahanati moja huko Shikuse,ilibainika kuwa mpendwa huyo alikuwa ameshaaga dunia.

Na kama ilivyoratibiwa,Mwili wa marehemu umepasuliwa leo ili kubaini chanzo cha tanzia hiyo,ambapo upasuaji umeonyesha Andrieta alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

ups

Ripoti ya uasuaji ilionyesha kuwa ,marehemu alikuwa na uvimbe kwenye moyo wake.Familia ya mpendwa huyo ilishuhudia upasuaji ikadhibitisha na mpasuaji kuwa marehemu hakuwa na tatizo lingine. Aidha juhudi zetu za kumpata mpasuaji huyo hazikufua dafu.Kwingneko,mumewe Andrieta hakufaulu kuongea nasi kwani alizidiwa na hisia ya kumpoteza mpendwa wake.

Familia hiyo sasa imeonyesha kutoridhika na matokeo hayo na inarai washikadau kwenye kijiji  hicho cha Mukhoya kuendeleza uchunguzi kulingana na ripoti hiyo ya kusikitisha hata baada ya upasuaji wa mwili wa mpendwa wao kukamilika.

Leave a Comment