Mazish yake iliwaleta pamoja viongozi Rais William Ruto,naibu wake Rigathi Gashaguana kiongozi wa Azimio RailaOdinga.Kiongozi wa taifa na kinara wa upinzani walionekana wakisalimiana hadharani hii ikiwa ni mara ya kwanza uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Ikumbukwe kuwa wawili hawa wamekuwa wakirushiana cheche zinazoonyesha tofauti zao kwenye ulingo wa siasa,huku kila mmoja akionekana kuvuta upande wake.
Akizungumza kwenye mazishi hayo Odinga amemtaka Rais kupungguzia wakenya mzigo badala ya kuwalimbikizia gharama ya ushuru wakati huu maisha yamekuwa magumu kwao.
Aidha,Rais William Ruto amemjibu Raila kuwa ni kweli uchumi wan chi umedorora,ila amemkosoa kuwa ni kutokana na muungano wake na serikali iliypita.Aidha ameahidi kuwa mapendekezo ambayo amepeleka bungeni ni ya kuwafaidi wakenya ila sivyo anvyosema Raila kuwa ni kuwanyanyasa wakenya.
Vilevile,Rigathi Gashagua kwa upande wake amelaumu hatua ya Azimio kuungana na serikali iliyopita kwani anasema ndio chanzo chanzo cha masaibu yote yanayokumba nchi.Anasihi upinzani kuipa nafasi serikali iliyopo iendelee na haraktiza kukomboa uchumi wa nchi ambao unatokomea.
Naye waziri mkuu Musalia Mudavadi ameitetea serikali kuwa ina juhudi za kukwamua uchumi wan chi ambao ulikuwa umezoroteshwa na serikali iliyopita.Amewarai viongozi wa Kenya kuungana ili kufanikisha ufanisi wa Taifa.
Kutokana na hotuba walizotoa viongozi hao,ni dhahiri kuwa bado nchi itaaendelea kushuhudia joto la siasa kwani,hata baada ya kuanza maongezi ya maridhiano,wameonekana kuendeleza tofauti zao kila kuchao.Ni juhudi za mwananchi sasa kufunga mkanda na kuona jinsi atakavyojiendeleza kimaisha,na kusubiri kufufliwa kwa nchi kama anavyoahidi rais William Ruto.