UpsNi vuta nikuvute inayoshuhudiwa kati ya serikali na viongozi wa Azimio kuhusu mswada wa fedha wa mwaka huu.Mswada huu umeonekana kuwakera washikadau wengi na muungano wa walimu Kuppet wanaodai serikali imewatenga katika kutekeleza ushuru wa asilimia kutozwa kwenye mshahara wao,ili kufanikisha mradi wa nyumba uliozinduliwa naye Rais William Ruto.UpsViongozi hao wanasema tayari wakenya wanakumbwa na tatizo la bei ghali ya bidhaa na hivyo kuwa vigumu kwao kuekeza katika ujenzi wa nyumba hizo.Serikali katika mpango huo inapanaia kujenga nyumba laki mbili ambazo Rais anasema zitasuluhisha swala la uhaba wa nyumba nchini.UpsAkizungumza akiwa kwenye hafla moja ya mazishi huko Murang’a, Raila Odinga amekashifu Rais William Ruto kwa kupuuza matakwa ya wakenya na badala yake kutaka kuwanyanyasa kupitia mswada wa ushuru wa aslimia tatu kwenye mishahara yao.UpsAnasema amechukua hatua hiyo bila kushauriana naye na kupuuza matatizo ya wananchi aliowaahidi kuwasaidia.Kauli hii imeungwa mkono na viongozi walioandamana naye akiwemo aliyekuwa gavana wa Muranga Mwangi wa Iria.upsKwingineko,katika hafla ya kuzindua kitabu cha waziri wa ulinzi Aden Dwale,Kinara wa walio wengi bungeni Silvano Sosoro akihakiki kuwa mswada huo wa ushuru wa asilimia tatu itafanikishwa bila ya kupingwa,na hivyo kelele za chura hazitamzuia tembo kunywa maji.UpsHayo yanaendelea wakati mazunguzo ya maridhiano yanaendelea.Kwenye vuta nikuvute hiyo,je kuna haja ya mazunguzo haya?Kuna maridhiano gani ikiwa viongozi wataendelea kurushiana cheche na kulimbikiziana lawama mauzngumzo ya maridhiano yanapoendelea?Je mkenya ana manufaa gani ikiwa viongozi watalazimisha kupitisha miswada kulingana na uwezo na nguvu zao?Ama kweli,fahali wawili wapiganapo,nyasi ndio huumia.

Leave a Comment