Kwenye shinikizo zao,wanawataka wabunge wote waikweo wa Kenya Kwanza wapinge mswada huo,Wanapinga marekebisho yoyote ati ndi o mswada huo upitishwe,na badala yake wanaitaka serikali iliyo mamlakani Kupunguza ushuru,Kupunguza matumizi ya pesa katika serikli kuu na mengine mengi
- Wabunge wapinge mswada na bajeti
- Mswada usifanyiwe marekebisho
- Ushuru upunguzwe
- Serikali ipunuze matumizi ya pesa
Muungano wa Azimio la Umoja umetoa shukrani kwa wabunge wa Azimio waliopiga kura kupinga Mswada wa Fedha wa 2023. Hii ni baada ya Wabunge 81 kati ya 257 kuupinga Mswada huo huku Wabunge 176 wakipiga kura kuuidhinisha katika awamu pili ya kusomwa hapo jana. Katika taarifa,Azimio walisema Wabunge hao 81 walizungumza kwa ajili ya mamilioni ya Wakenya waliokandamizwa.
Azimio wakati wote imeelezea matumaini yake kwamba angalau bado maji hayajazidi unga baada ya hata baaada ya Kenya Kwanza kuibuka mshindi.Wabunge wa Azimio katika Bunge hilo waliamua kuimba wimbo maarufu wa ‘Bado mapambano’ baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi naspika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula.
Mswada huo sasa unapania kupitia kwa kamati ya Bunge ambapo wajumbe watakuwa na nafasi ya kuchunguza mswada huo kina kwakina.Kamati itakaopitia Mswada huo kifungu baada ya kifungu ,iwabunge watapiga kura kwa kila pendekezo.
Miongoni mwa marekebisho muhimu ya Mswada huo ni asilimia 15 iliyopendekezwa kwenye sanaa za dijitali ambapo ushuru umepunguza kutoka asilimia 15 hadi asilimia 5. Ushuru wa nyumba uliopendekezwa wa asilimia tatu pia umepunguzwa hadi asilimia 1.5 katika marekebisho hayo.
Kabla ya kura hiyo, Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga walikuwa wametoa taarifa kwa wajumbe wa mirengo yao wakisema watakuwa chini ya shinikizo zao kuhusu mswada huo.